KUMBE LA GALAXY WALIMTAKA LAMPARD KABLA YA GERRARD - LEKULE

Breaking

28 Jun 2015

KUMBE LA GALAXY WALIMTAKA LAMPARD KABLA YA GERRARD

Kocha wa timu ya LA Galaxy inayoshiriki ligi kuu soka nchini Marekani, Bruce Arena ametoboa siri kwamba nia yao ilikuwa ni kumsajili mchezaji Frank Lampard kabla hawajabadili maamuzi ya kumsajili mkongwe mwingine toka klabu ya Liverpool Steven Gerrard.
“Tulikuwa na lengo, na tulishaanza mazungumzo na Chelsea hata kabla ya Lampard kwenda kuchezea kwa mkopo kwenye klabu ya Manchester City lakini ilishindikana na wenzetu New York City walituwahi mwisho wao wakafanikiwa kumnyakua Lampard”,alisema kocha Bruce Arena wakati akifanya mahojiano na mtandao wa dailymail toka nchini Uingereza.

No comments: