BAD BOYS BACK AGAIN SOON - LEKULE

Breaking

28 Jun 2015

BAD BOYS BACK AGAIN SOON

Kundi la muziki wa hiphop toka nchini Marekani lililowahi kuvuma kipindi cha miaka ya nyuma linatarajiwa kurudi upya na kufanya kazi tena kwa pamoja.
Kundi hilo lililowahi kuongozwa na marehemu rapa Notorious B.I.G.likiwajumuisha wanamuziki kama P Diddy, Lil’ Kim, Faith Evans, Ma$e na wengine kwa sasa lipo kwenye mazoezi mazito, na jumapili ya june 28 wataperform kwenye jukwaa la tuzo za BET.
Mwanamuziki Faith Evans, amepost kipande cha video kwenye akaunti yake ya instagram kikimuonyesha yupo na crew wakiwafanya mazoezi ya kuimba, na kuandika caption yenye maneno yafuatayo.
“Love Like This” with her dancers and choreographer Laurieann Gibson. “Creative Flow #BET awards #prepnation #history coming,” .

Ikumbukwe mwezi wa nne mwaka huu kiongozi wa kundi hilo kwa saa, P Diddy alitangaza kwamba Bad Boys wanarudi tena, na kusema pia kutakuwa na ziara ya kundi hilo sehemu tofauti duniani, ikiitwa kwa jina la Bad Boys Tour.

No comments: