Kiongozi wa mashtaka nchini Misri
Hisham Barakat ameuawa kutokana na majeraha aliopata baada ya bomu
kulipua gari lake mjini Cairo.
Msafara wa Bwana Barakat ulishambuliwa ulipokuwa ukipitia katika wilaya ya Heliopolis.Nguvu za shambulio hilo ziliharibu baadhi ya nyumba na maduka.Walinzi wawili wa bwana Barakat pia walijeruhiwa.
Bwana Barakat amekuwa akipendekeza mamia ya wapiganaji hao kufunguliwa mashtaka tangu kupinduliwa kwa rais aliyepinduliwa , Mohamed Morsi, mwaka 2013.
Kundi linalojiita Popular Restistance of Giza limekiri kutekeleza shambulizi hilo.
No comments:
Post a Comment