Idhaa ya Kiswahili ya BBC Swahili itazindua sura mpya ya “Dira ya Dunia” leo!
Kipindi
hicho kinachopeperusha taarifa ya habari kwa zaidi ya watazamaji
milioni 6.9 itakuwa na sura mpya inayojumuisha maandishi mapya
yaliyotiwa nakshi,vipindi vipya na ripoti za kina zinazojumuisha habari,
michezo na burudani.Tangu ilipozinduliwa mwaka wa 2012 Dira ya Dunia TV, inatazamwa kila siku na mashabiki kanda ya Afrika Mashariki na Kati matika mataifa ya Tanzania, Kenya, Burundi na katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Aidha “Dira ya Dunia” ina mashabiki si haba katika mitandao ya kijamii.
Mtangazaji nyota wa idhaa hii ya Kiswahili, Salim Kikeke, alitunukiwa mataji ya ''Tuzo Za Watu'' na Mtangazaji bora wa runinga wa mwaka, kwa mwaka wa pili mtawalio.
Mshindi wa tuzo hizo anachaguliwa na umma.
Kikeke anasaidiana na watangazaji wenza, Kassim Kayira, Zuhura Yunus na Peter Musembi.
Dira Ya Dunia yenye sura mpya itaendelea kuwaletea wageni wenye uzoefu wa maswala tofauti.
Wageni waliohojiwa tayari katika Dira ya dunia ni pamoja na rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, rais Pierre Nkurunziza wa Burundi na rais Yoweri Museveni wa Uganda mbali na wasanii waliobobea kama vile Diamond Platnumz kutoka Tanzania, Eddy Kenzo kutoka Uganda na Juliani wa Kenya.
“Siamimi kwa hakika kuwa imekuwa takriban miaka mitatu tayari .
''Imekuwa safari ya kuvutia sana.''
''Mapokezi yetu katika kanda zima ya Afrika Mashariki na kati ni ya kufana na kuridhisha.''
''Tunapania kuendelea kuwapasha habari wasikilizaji wetu kuwa elimisha na pia kuwa burudisha kwa miaka mingi.''
''Hii sura tunayoizindua ni thibitisho tosha kuwa ari yetu ni hiyo'' anasema mtangazaji kinara Salim Kikeke.
Kwa upande wake Mhariri na Mtayarishi mkuu wa Dira ya Dunia Tv bi Mariam Omar anasema kuwa
''inafurahisha mno kwa mtazamaji kuwa tunaimarisha kipindi chetu maarufu ''Dira ya Dunia TV .''
''Tutaendelea kuwapa watazamaji wetu habari za utendeti zaidi na kwa njia za kuvutia watazamaji wetu ambao bila shaka watakuwa na uwezo zaidi wa kuwasiliana nasi na kuchangia habari tutakazo peperusha.''
No comments:
Post a Comment