Ripoti kutoka Somalia zinasema kuwa
kundi la wapiganaji wa jihad nchini humo Al Ashabaab limevamia kambi
moja ya kijeshi na kuwaua takriban wanajeshi 10.
Walioshuhudia wanasema kuwa kulikuwa na mapigano makali karibu na kambi hiyo katika mji wa bandari wa Kismayu.Alshabaab limeimarisha mashambulizi yake dhidi ya wanajeshi wa Somalia na wale wa Umoja wa Afrika wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Wakaazi wa jimbo la kusini mwa Lower Shebelle wanasema kuwa vikosi vya Umoja wa Afrika vimejiondoa katika kambi zake katika maeneo hayo.
Kufikia sasa hakuna tamko lolote kutoka kwa jeshi la umoja huo.
No comments:
Post a Comment