Je,unaweza kuishi ukiwa uchi? - LEKULE

Breaking

29 Jun 2015

Je,unaweza kuishi ukiwa uchi?

Watu wengi wasingejihisi vyema kuvua nguo zao zote na kusalia uchi wa mnyama katika maeneo ya uma,lakini kwa wengine ni maisha yao.
Mwandishi kutoka nchini Marekani Mark Haskel Smith alikabiliana na changamoto zote na kuweza kuishi bila nguo.Iwapo upo katika uwanja wa ndege ,huwezi kufanya masihara kuhusu bomu.
Na iwapo uko na watu walio uchi huwezi kufanya masihara kuhusu matiti.
Na mungu wangu,usisisimkwe,utaamrishwa uondoke asema Haskell Smith.

Haya ni mambo mawili aliyogundua alipotembelea maeneo ya kupumzika ya watu walio uchi duniani.

Ziara yake ya kwanza ilikuwa katika mkahawa wa Desert Sun Resort huko Palm Springs Carlifonia.

'Nilishtuka'.'Nilikuwa na wasiwasi katika chumba changu cha hoteli,nikijipaka mafuta baada ya mafuta hadi nilipotoka nje,nilikuwa niking'ara sana'',.
''Kuna watu chungu nzima katika kidimbwi cha maji wwaliokuwa ndani ya kidimbwi kimoja cha maji walioniangalia na kujifunika nyuso zao.
Nilijihisi vibaya sana,nilifikiri watu hawa wamenipita na zaidi ya miaka 20 lakini nilipojiangalia chini ''ooh mungu wangu''.
Baada ya kuzuru eneo hilo alizuru maeneo mengine ya watu walio uchi barani Ulaya.

No comments: