Mwanariadha wa mbio fupi Justin
Gatlin ameweka mda bora zaidi katika mbio za mita 200 na kuwa wa tano
duniani aliposhinda mbio hizo nchini Marekani.
Raia huyo wa
Marekani mwenye umri wa miaka 33 ambaye amehudumia marufuku mbili za
utumiaji wa dawa za kusisimua misuli aliweka rekodi ya mda wa sekunde
19.57 mjini Oregon.Rekodi hiyo imeifuta ile ya sekunde 19.68 aliyoiweka mnamo mwezi May wakati huo ikiwa rekodi bora duniani.
''Nilitaka kutoka ili niweke historia,na hivyo ndivyo nilivyofanya'',alisema Gatlin.
Gatlin ndiye mwanariadha wa mbio fupi aliyetawala mwaka 2015 baada ya kuweka rekodi bora mwaka huu ya sekunde 9.74 katika mbio za mita 100.
No comments:
Post a Comment