Dar es Salaam.
Ziara ya kwanza ya Rais wa Msumbiji, Filipe Nyussi nchini imefanikisha kusainiwa kwa mkataba wa kuondoa malipo ya viza kwa wanadiplomasia, wafanyabiashara na wananchi baina ya nchi hizo mbili.
Ziara ya kwanza ya Rais wa Msumbiji, Filipe Nyussi nchini imefanikisha kusainiwa kwa mkataba wa kuondoa malipo ya viza kwa wanadiplomasia, wafanyabiashara na wananchi baina ya nchi hizo mbili.
Mkataba huo mpya ulisainiwa
jana kati ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Msumbiji, Jaime Basilio
Monteiro na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania aliyewakilishwa na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya mazungumzo kati ya Rais Nyussi na mwenyeji wake, Jakaya Kikwete, Ikulu jijini hapa.
Akizungumza
kuhusu makubaliano hayo, Membe alisema kuanzia sasa wananchi wa pande
zote mbili watafaidika na uhusiano mwema uliojengwa kwa muda mrefu na
fursa za biashara kutoka nchi hizi.
“Hakutakuwa tena na
viza kwa Watanzania wanaokwenda Msumbiji. Awali, walilazimika kulipa
Dola za Marekani 900 (zaidi ya Sh1.8 milioni) kwa muda wa siku 30 wakati
wao walikuwa wanalipa Sh10,000 kwa siku 90. Baada ya mkataba huu,
hakutokuwa tena na malipo hayo,” alisema Membe.
Waziri
Membe alifafanua kuwa mkataba huo umeondoa pia malipo ya viza kwa muda
huo kwa wafanyabiashara, wanadiplomasia pamoja na wananchi wa kawaida
lakini wanafunzi wamepewa kipaumbele cha pekee kwani hawatotakiwa kulipa
kwa muda wote wa masomo yao.
Alisema uhusiano wa muda
mrefu baina ya nchi mbili hizi, umechangia kwa kiasi kikubwa kufikia
uamuzi huo na katika siku zijazo, wanatarajia kufanya mazingira ya
kuvuka mipaka yasiwe kikwazo kwa maendeleo ya wananchi wake.
Rais
Nyussi aliwasili nchini jana na atafanya ziara ya siku tatu
itakayomfikisha pia Zanzibar ambako atazungumza na Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Dk Ali Mohammed Shein kabla ya kuelekea
Dodoma ambako atatembelea Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kabla ya
kulihutubia Bunge.
No comments:
Post a Comment