RICK ROSS ACHIMBWA MKWARA KUTUMIA PICHA ZA JAY Z - LEKULE

Breaking

18 May 2015

RICK ROSS ACHIMBWA MKWARA KUTUMIA PICHA ZA JAY Z


Rapa Rick Ross ‘Ricky Rozay’.

New York, Marekani
MPIGA picha maarufu nchini Marekani, Armen Djerrahian, anaweza kujikuta katika vita ya maneno na rapa Rick Ross ‘Ricky Rozay’ baada ya kumpiga mkwara rapa huyo juu ya matumizi ya picha za Jay Z.Ross na Jay Z wamekuwa ni marafiki wa muda mrefu huku wakishirikiana kufanya kazi kadhaa pamoja.

Mpiga picha maarufu nchini Marekani, Armen Djerrahian.

Lakini Djerrahian ambaye ni mpiga picha wa Jay Z, amemshupalia Ross na kumueleza kuwa hata kama yeye ni rafiki wa rapa huyo mmiliki wa lebo ya Roca Fella lakini haruhusiwi kutumia picha zake bila idhini.Djerrahian, alifikia hatua hiyo baada ya Ross kutupia picha ya Jay Z ambayo ilipigwa 2003 kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram.

Djerrahian alifika mbali baada ya kumlaumu Ricky Rozay ambaye aliitumia picha hiyo kwenye video ya wimbo mpya wa "Movin Bass" ambao amemshirikisha Jay Z.

No comments: