Kahama.
Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga inawashikilia watu watano, akiwamo mwalimu wa shule ya msingi na mwanamke mmoja, kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya albino wakiwa katika harakati za kutaka kuviuza wilayani Nzega na Kahama.
Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga inawashikilia watu watano, akiwamo mwalimu wa shule ya msingi na mwanamke mmoja, kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya albino wakiwa katika harakati za kutaka kuviuza wilayani Nzega na Kahama.
Tarifa
ya kamanda wa polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Jastus Kamgisha iliyotolewa
kwa waandishi wa habari mjini hapa jana na Mkuu wa polisi wilayani hapa,
Leonard Nyandahu, watu hao walikamatwa saa 7:00 mchana katika nyumba
moja ya kulala wageni inayofahamika kwa jina la Maji Hoteli iliyopo
Phantom, Kata ya Nyasubi.
Nyandahu alimtaja mwalimu
huyo kuwa ni Bahati Kirungu (56) anayefundisha katika Shule ya Msingi ya
Katungulu iliyoko Kata ya Wendele na mwanamke anayeitwa Regina Kashinje
(40) ambaye ni mkulima na mkazi wa Isagehe, Nzega.
Wengine
ni Mhoja John (24) mkulima na mkazi wa Isagehe Nzega, Bilia Busanda
(39) mkulima na mkazi wa Mogwa Nzega, Shija Makandi (60) mkulima na
mkazi wa Isagehe Nzega na Aboubakary Ally (25) ambaye ndiye mtunza siri
ya watu hao ambaye ni mkulima na mkazi wa Isagehe Nzega.
Nyandahu
alidai kuwa Mei 19, asubuhi, mkuu wa upelelezi wa kituo cha polisi
wilayani Nzega alipata taarifa kuwa kuna mtu anauza viungo vya albino,
ndipo walipoweka mtego. Hata hivyo, alidai kuwa walishindwa kuwakamata
na baadaye mtu huyo alihamishia biashara hiyo wilayani Kahama.
Nyandahu
alisema maofisa upelelezi wa Tabora kwa kushirikiana na ofisa upelelezi
wa Kituo cha Polisi cha Kahama, walifuatilia nyendo za watu hao na
wakaweka mtego mwingine wa kuwakamata uliofanikiwa kuwanasa.
Hata
hivyo, polisi wilayani Kahama wanaendelea kuwashikilia watu hao kwa
mahojiano zaidi ikiwa ni pamoja na kuubaini mtandao wao.
Kukamatwa
kwa watu hao kumekuja wakati Serikali ikiwa katika mikakati ya
kudhibiti mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambao wameanza kusakwa
tena mwaka huu baada ya vitendo hivyo kutulia kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment