Hii ni mara ya kwanza nakutana na Lady Jaydee na kumfanyia interview
ndefu. Kwangu nimeichukulia kama heshima kubwa kwa mwanamuziki huyu
mkongwe kuamua kutafuta muda na kuja kuchill na mimi.
Kabla sijaanza kuongea naye, namuambia Lady Jaydee kuwa hii itakuwa
interview ‘positive’ zaidi kuwahi kuifanya katika miaka ya hivi
karibuni.
“Sisi kwetu tumezaliwa watoto kumi,” anasema Jaydee. “Lakini bahati
mbaya watatu wamefariki na tumebakia saba. Familia yetu ni familia ya
dini, tumezaliwa kwenye maadili ya kisabato, tumekulia kanisani na
nidhamu.”
“Nilikuwa naimba kwaya kanisani, nilishiriki pia kwenye vikundi vya
Pathfinder kanisani kwetu tangu nina miaka saba yaani nilikuwa naweza
nikasimama mbele ya kanisa nikaongoza watu, nikaimbisha watu wakaimba.
"Unajua ukiwa mdogo huwezi ukajua kama ni kipaji, mimi nikawa naona ni
kitu tu ambacho napenda, kwahiyo nikawa nafanya tu for fun.”
Jaydee anasema alikuwa ni mtoto msikivu na aliyekuwa akifuata kile
alichokuwa akielekezwa na wakubwa zake. “Muda mwingi nilikuwa nautumia
kanisani zaidi, kwahiyo ilikuwa ni shule, kanisani,” anakumbuka.
Anasema tangu alipojitambua, muziki kilikuwa ni kitu alichopenda kuja kukifanya kama kazi yake.
“Nilikuwa napenda kuwaangalia watu ambao wanaimba na kujiweka kwenye
viatu vyao na kujifikiria vipi mimi nikiwa kama yule, sikuwa najiona mtu
mwingine zaidi ya mwanamuziki.”
Lady Jaydee alizaliwa mkoani Shinyanga hadi darasa la nne kabla ya
kuhamia jijini Dar es Salaam. Akiwa Dar es Salaam, pamoja na kuwa na
ndoto ya kuja kuwa mwanamuziki, alijikuta katika wakati mmoja akifanya
kazi kama mtangazaji wa redio.
“Saa zingine nilikuwa najaribu kutangaza TV kwahiyo nakaa kwenye kioo
najiangalia najaribu kuona kama naweza kuwa presenter.
"Kwahivyo
nikasema ngoja nikajaribu kuomba labda kwenye redio pia nione kama
ntaweza, lakini mwenyewe binafsi siamini kama ni mtangazaji.
"Ila
nafikiri nilikuwa naenda kwasababu napenda muziki na naona ndio sehemu
ambayo naweza nikakutana na watu ambao tunaweza tukafanya masuala hayo
ya muziki na vitu kama hivyo.”
“Nilifanya ile kazi lakini sio kwamba nilikuwa naipenda sana
kwasababu sio passion yangu. Baadaye nilipoweza kufanya muziki nikaona
siwezi kuendelea na kitu ambacho hakipo kwenye moyo wangu, nikaona
nifanye muziki na niache kutangaza.”
Wimbo wa kwanza Lady Jaydee kurekodi uliitwa ‘Sema Unachotaka’
aliourekodi kwenye studio za Master J baada ya kushinda shindano
lililoandaliwa na Radio One Stereo.
Wimbo huo uliwekwa kwenye album iitwayo Asubuhi iliyokuwa na nyimbo za wasanii wengine pia.
Album yake ya kwanza ilikuwa ni Machozi iliyokuwa na nyimbo nyingi za
huzuni na kuumiza japo anasema hiyo haikuashiria kuwa hayo ndio
yalikuwa maisha yake.
Kabla ya kuwa na jina, Jaydee alikuwa akirap na Dr. Dre ambaye hadi
leo ni role model wake, alikuwa mmoja wasanii aliokuwa akiwasikiliza
sana. Ndoto yake hadi leo ni kuja kurekodi na producer huyo.
“Siku zote tu nimekuwa nikiwish tu kwamba labda kama angeweza kunitengenezea hata wimbo mmoja,” anasema Jaydee.
Maisha ya umaarufu yamekuwa na changamoto nyingi kwake ikiwemo
kujizuia kufanya mambo anayoyapenda ambayo kama asingekuwa staa
angeyafurahia kuyafanya.
“Watu wanashindwa kuelewa kwamba mimi ni Jaydee sawa lakini mimi ni Judith na ni binadamu wa kawaida.” anasisitiza.
“Naweza kukasirika, naweza kucheka, naweza kulia, naumia kama mtu
mwingine anavyoumia. Lakini wao wanavyochukulia ni kwamba unavyokuwa
pale wanapokuwa wameshakufahamu, hutakiwi vitu vingine kufanya kwahiyo
unakuwa saa zingine hauko huru sana.
"Labda mtu amekuja amekuchokoza
inabidi umwache tu hauwezi kumrudishia wakati katika hali ya kawaida mtu
yeyote anaweza kufight back.
"Na mimi ni mgomvi sana na huwa sipendi
kuonewa, saa zingine unaweza kukuta mtu akakufanyia kitu lakini ukakaa
tu kimya, huyo sio mimi lakini inabidi tu nifanye hivyo.”
No comments:
Post a Comment