Balozi Liberata Mulamula Ateuliwa Kuwa Katibu Mkuu Wa Wizara Ya Mambo Ya Nje Na Ushirikiano wa Kimataifa - LEKULE

Breaking

5 May 2015

Balozi Liberata Mulamula Ateuliwa Kuwa Katibu Mkuu Wa Wizara Ya Mambo Ya Nje Na Ushirikiano wa Kimataifa

<
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Balozi Liberata Rutageruka Mulamula kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kwa sasa Balozi Mulamula ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico.

Rais Kikwete pia amemteua Balozi Hassan Simba Yahya kuwa naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kwa sasa Balozi Yahya ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizarani hapo.

Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2015
Mwisho

Imetolewa ;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
4 Mei, 2015

No comments: