Waziri Mkuu, Mizengo Peter Pinda ameunda kamati maalumu ya kudumu ya
kusimamia Usafiri wa barabarani nchini ili kutatua changamoto
zinazoikabali sekta ya Usafiri.
Katika kamati hiyo mwenyekiti
wake atakuwa katibu mkuu wa wizara ya chukuzi, Katibu akiwa kamishna wa
polisi barabarani na Mkurugenzi wa SUMATRA huku wajumbe wakiwa ni pamoja
na katibu mkuu wizara ya kazi ya na ajira, katibu mkuu ujenzi,
mwanasheria mkuu wa serikali na naibu katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu.
Mkuu
wa ratibu wa idara ya maafa toka ofisi ya waziri mkuu, mwenyekiti wa
TABOA na TATOA, CHAKUA nao wanatakiwa kuanza kufanya vikao leo na kila
mwezi watakutana kujadili na kutatua changamoto zote kasoro zile za
kisheria ambazo zitapelekwa serikalini kwa mchakato zaidi wa
kuzirekebisha.
Wakati huo huo umoja wa vyama vya madereva nchini
Tanzania umesema hauna taarifa juu ya wao kutakiwa kukutana na waziri
mkuu Mh. Mizengo Pinda kwa ajili ya mazungumzo kama inavyozungumzwa na
kusisitiza kuwa wao wataendelea na mgomo wao ulioanza leo mpaka masuala
yao yatapofanyiwa kazi.
Akizungumza na East Africa Radio leo
Makamu Mwenyekiti wa Muungano wa vyama vya Madereva Abdallah Lubala
amesema kauli ya kuwa wamekubaliana kukutana na Mh. Pinda ni za kisiasa
na hazina ukweli wowote hivyo wataendelea na mgomo wao.
Wakati
huo huo mgomo huo ambao umetangazwa kwa nchi nzima athari zake
zimejitokeza katika mikoa mingine tofauti ambapo madereva wa mabasi ya
abiria wamegoma huku wasafiri wakitumia usafiri mbadala wa bajaji pamoja
bodaboda.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa
jiji la Mbeya, Arusha na Mwanza wamesema kuwa wanalazimika kutembea
umbali mrefu kwenda makazini na wangine wakitumia gharama kubwa kutokana
na vyombo hivyo wanavyotumia kupandisha bei za nauli kuliko kawaida.
No comments:
Post a Comment