Mwanajeshi wa JWTZ Ajinyonga Jijini Mwanza - LEKULE

Breaking

9 Apr 2015

Mwanajeshi wa JWTZ Ajinyonga Jijini Mwanza




Fundi wa magari wa Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi namba 512 MTC Nyegezi, jijini Mwanza, Jacob Mponeja (55) amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya katani huku akiacha ujumbe.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Joseph Lusungu tukio hilo lilitokea Aprili mosi mwaka huu majira ya saa moja asubuhi.

Alisema ujumbe huo ulioandikwa kwenye kitabu kidogo kilichokutwa kwenye eneo la tukio ulisomeka; “Kifo changu kimetokana na mke wangu kujihusisha na vitendo vya kishirikina, hali iliyosababisha kutaka kuuawa mara mbili na mtu asilaumiwe kwa kifo changu.”

Alisema kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, ambaye ni mwanafunzi katika sekondari ya Nyabulogoya, kabla ya tukio la kujinyonga, baba na mama yake Happy Mabula (45), walikuwa na ugomvi mkubwa.

Kaimu Kamanda huyo alisema katika ugomvi huo mama huyo alikatwa shoka na mumewe na kwamba alikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu na kwamba hali yake sio nzuri.

Alisema katika eneo la tukio kulikutwa shoka lililokuwa na damu pamoja na kitabu hicho kidogo kilichokuwa na ujumbe ulioandikwa na marehemu.

No comments: