Mwenyekiti mtendaji wa IPP DR. REGINALD MENGI ameeleza kushtushwa na taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la taifa imara zikimtuhumu kuwa ana nia ya kutaka kuiangusha serikali ya Rais Kikwete na kumshughulikia baada ya kumaliza muda wake wa uongozi kunyamaziwa na ikulu na idara ya habari maelezo kwa wiki tatu bila kutoa ufafanuzi wowote.
Katika kauli yake kwa vyombo vya habari Dr. Mengi amesema taarifa ya Gazeti hilo iliyouliza swali ,ZITTO AMCHONGEA MENGI KWA JK ambayo pia imesema Rais Kikwete aliapa kupambana naye inampa hofu kubwa kuhusu mustakabali wa maisha yake kutokana na kuachwa kuendelea kusambaa kwa tuhuma hizo.
Amesema ukubwa wa hofu hiyo ni kutokana na Rais ambaye ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama kauli yake kama ilivyonukuliwa na Gazeti kuwa atapambana naye inaweza kuchukuliwa kama agizo kwa vyombo vya dola kumuangamiza.
No comments:
Post a Comment