19 wafa mgodini Kahama. - LEKULE

Breaking

18 Apr 2015

19 wafa mgodini Kahama.



Wachimbaji wadogo wadogo 19 wa dhahabu wamefariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi kufuatia wa mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kubomoka kwa mashimo hayo katika kijiji cha Karore,Kata ya Runguya,tarafa ya Msalala Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyang a.

Kamanda wa polisi mkoani humo,JUSTUS KAMUGISHA a mesema kwa siku za karibuni wachimbaji hao wali acha kuchimba kutokana na machimbo yalikuwa hayaonekani,lakini juzi kuna mchimbaji mmoja aliona kuna dalili za kuonekana kwa machimbo hayo na ndipo akawapigia wenz ake simu kwa ajili ya kwenda kuanza shughuli za uchimbaji lakini ilivyofika jana shughuli hizo zilisitishwa.

Kwamujibu wa Kamanda KAMUGISHA,usiku wa kuamkia leo kuna wachimbaji ambao walivavamia machimbo hayo ambayo yalishaachwa kuchimbwa muda mrefu na ndipo wakaanza shughuli ya uchimbaji kutokana na machimbo hayo kuonekana kutokuwa imara na mvua iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo yakabomoka na kuwafukia na kusababisha vifo vyao.

Amesema miili tayari imeshat olewa kutoka kwenye mashimo hayo,lakini bado wanaendelea na juhudi za kuangalia kama kuna miili mingine imebakia.

No comments: