Dar es Salaam.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewaaga rasmi wabunge baada ya kuvuliwa uanachama wa Chadema na kuahidi kuwa “Mungu akipenda” atakuwa tena ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria Novemba.
“Ni uamuzi mgumu ambao imebidi niukubali kwa matakwa ya chama,” alisema Zitto alipopewa nafasi 3:14 muda mfupi kabla ya Bunge kumaliza shughuli zake za jana.
Tulifurahi pamoja, tulilia pamoja, na tulicheka pamoja. Naondoka na Mungu akipenda tutakutana tena tutaonana Novemba,” aliongeza mbunge huyo ambaye alisifu kuwa sehemu ya Bunge la Tisa ambalo alisema lilijenga misingi ya chombo hicho kuwa na meno ya kuisimamia Serikali.
Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alitangaza machi 10 mwaka huu kuwa Zitto amejivua rasmi uanachama kutokana na kitendo chake cha kufungua kesi mahakamani kutaka katibu mkuu wa Chadema ampe nyaraka za mwenendo wa vikao vya Kamati Kuu vilivyomvua madaraka yote, kitu ambacho ni kinyume cha Katiba ya chama hicho kikuu cha upinzani.
Lissu alitoa tamko hilo saa chache baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali shauri la Zitto kutokana na kutofuata taratibu zinazotakiwa kulifungua mahakamani.
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu alieleza kusikitishwa na uamuzi huo wa Zitto, akisema anawaacha wabunge wenzake katika kipindi kigumu.
“Ni simanzi kubwa kutuacha peke yetu katika kipindi hiki kigumu. Ushauri wako tutaukumbuka. Umetambulika kimataifa na kitaifa utatambulika pia,” alisema Zungu.
Zitto, ambaye alikuwa pia mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, alijipatia umaarufu wakati wa Bunge la Tisa kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja, hasa kwenye masuala ya mikataba ya madini.

No comments:
Post a Comment