Tamko la wana Jangwani-Yanga - LEKULE

Breaking

4 Mar 2015

Tamko la wana Jangwani-Yanga

Uongozi wa klabu ya Yanga ya Jijini Dar es salaamb umesema baada ya kufanya uchunguzi wa kina hatimaye umebaini mambo mbalimbali yanayofanyika chini ya Bodi ya ligi inayosimamia ligi kuu ya soka ya Tanzania bara.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika Makoa makuu ya klabu hiyo mapema Asubuhi ya leo march 3 /2015 Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano klabu hiyo Jerry Muro amesema mpaka sasa wamefanikiwa kubaini maswala mbalimbali ambayo bodi ya ligi imeshindwa kuyasimamimia ipasavyo ikiwemo upotoshwaji wa Taarifa za kuahirishwa kwa mchezo wao dhidi ya Jkt Ruvu ambao ulikuwa uchezwe leo , ambapo kaimu Afisa mtendaji wa bodi ya Ligi Fatma Abdalah amekuwa akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari kuwa uongozi wa Yanga ulipewa taarifa ya kuarishwa kwa mchezo wao kupitia njia ya barua pepe tangu tarehe 16/02/2015 , Taarifa ambayo uongozi wa Yanga umeikataa.

Uongozi huo pia umepinga swala la mchezaji wa Timu ya Simba Ibrahim Hajib Migomba kuhusiana na kadi za njano alizopata mchezaji huyo kabla hajaruhusiwa kuitumikia Timu yake katika mchezo ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Yanga , ambapo yanga imebaini kuwepo kwa taarifa za upotoshwaji kuwa mchezaji huyo alipata kadi za njano Nne na sio kadi Tatu kama ilivyoelezwa na Bodi ya Ligi,

Mechi ambazo mchezaji huyo alipatiwa kadi za njano ni Mchezo No 17 uliofanyika tarehe 4/10/2015 kati ya Simba dhidi ya Stand United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam , mchezo mwingine ni mchezo No 99 uliofanyika tarehe 15/02/2015 kati ya Polisi morogoro dhidi ya Simba katika uwanja wa Jamhuri mjini morogoro, mchezo No 108 ulichezwa tarehe 22/02/2015 kati ya Stand United dhidi ya Simba katika uwanja wa kambarage mjini shinyanga , Pamoja na mchezo No 125 wa tarehe 28/02/2015 kati ya Simba dhidi ya Tanznia Prisons.

Uongozi wa Yanga pia umetoa mapendekezo na kulitaka shirikisho la soka la Tanzania kupitia Rais wake Jamal Malinzi kuvunja kamati ya ligi,na pia umemtaka kaimu Afisa mtendaji wa bodi ya ligi Fatma Abdalah kujiuzulu kutokana na kupotosha sheria na Taratibu , vinginevyo wao kama Yanga hawatakuwa tayari kupeleka Timu uwanjani tarehe 11/03/2015 dhidi ya Jkt Ruvu.

No comments: