Ferguson:Meya awaadhibu Polisi - LEKULE

Breaking

5 Mar 2015

Ferguson:Meya awaadhibu Polisi

Meya wa mji wa Ferguson, jimboni Missouri, ametangaza hatua kadha wa kadha zitakazochukuliwa kufuatia ripoti iliyoonyesha ushahidi dhidi ya polisi wa mjini humo kujihusisha na vitendo vya ubaguzi wa rangi.

James Knowles amesema mwajiriwa mmoja toka Idara ya Polisi amefukuzwa kazi na wengine wawili wamelazimishwa kwenda likizo baada ya kushutumiwa kutuma barua pepe yenye ujumbe wa kibaguzi.

Knowles amewaambia waandishi wa Habari kuwa Idara itaongeza namba ya Maafisa wasio wazungu na kujikita katikamafunzo.

Meya ametoa kauli hiyo baada ya Wizara ya Sheria kufanya uchunguzi kuhusu kifo cha kijana mmoja mweusi aliyeuawa mjini Ferguson na kubaini kuwa kulikuwa na viashiria vya ubaguzi wa rangi wakati wa tukio hilo.

No comments: