Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amekiri kuwa hajui ni mda gani itamchukua nyota wake Angel di Maria kuzoea maisha katika kilabu hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ameshindwa kuonyesha hali ya mchezo uliomfanya kupata uhamisho hadi kilabu hiyo ya Old Trafford kwa kitita cha pauni millioni 59.7 wakati wa kipindi cha uhamisho cha mwezi Julai na Agosti ,lakini Van Gaal anahisi kwamba raia huyo wa Argentina si mchezaji pekee anayejaribu kuzoea maisha katika kilabu hiyo.
Mkufunzi huyo raia wa Uholanzi ametaja uzoefu wake katika ligi nyengine za Ulaya akisema kuwa ni mambo ya kawaida kwa wachezaji wapya kuchukua hadi mwaka mmoja kwa wao kuzoea mazingira mapya.
Alipoulizwa ni hadi lini anadhani itamchukua Di Maria kuzoea,Van Gaal alisema ''ni mwaka mmoja kwa jumla. Lakini huwezi kutoa jibu la jumla''.
''Ni rahisi kusema hivyo lakini siwezi kuthibitisha
''Nadhani ni wachezaji wote ambao tumenunua ,msimu wa kwanza huwa mgumu.Nilielezea hilo katika mkutano na wanahabari baada ya mechi dhidi ya Sunderland''.
''Kwangu mimi ni swala la kushangaza ,na ni swala la kushangaza zaidi iwapo Di Maria angezoea haraka.Unaweza kuona kwa kila mchezaji tuliyemnunua''.
Luke Shaw,Daley Blind,Anders Herrera,Radamel Falcao na Di Maria.
No comments:
Post a Comment