Padre feki kutoka jimbo la New York nchini marekani anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani morogoro. - LEKULE

Breaking

8 Mar 2015

Padre feki kutoka jimbo la New York nchini marekani anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani morogoro.



Jeshi la polisi mkoani morogoro linamshikilia mtu mmoja Joseph Asenga mwenye umri wa miaka 47 kwa tuhuma za kujifanya kuwa ni Padre wa kanisa katoliki na hata kuendesha ibada.
Taarifa zilizothibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa morogoro,Leonard Paulo, zimebainisha mtuhumiwa huyo kutiwa mbaroni katika maeneo ya modeko katika kanisa katoliki la Mt.Maria ambapo anadaiwa kuwahi kufika kanisani hapo kati ya mei na juni mwaka jana,kabla ya kurudia tena hivi karibuni, akijitambulisha alikuwa padri kwa kutoa vitambulisho feki akisema ametokea jimbo la NEW YORK nchini marekani na alikuja nchini kwa mapumziko na katika upekuzi amekutwa na majoho saba ya kipadri.

Katibu wa kanisa katoliki, jimbo katoliki la morogoro,Padre Lutsfud Makseyo,amesema amelaani tukio hilo na kwamba limewasikitisha na kuwahuzunisha kama kanisa,na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kuwafichua watu wote wanaofanya vitendo vya kitapeli kwa kujihusisha na uongozi wa kiimani.

No comments: