Wanawake nchini wametakiwa kuunga mkono katiba iliyo pendekezwa - LEKULE

Breaking

8 Mar 2015

Wanawake nchini wametakiwa kuunga mkono katiba iliyo pendekezwa





Wanawake nchini wametakiwa kuunga mkono na kuipitisha katiba iliyo pendekezwa kwa asilimia mia moja kwani imezingatia maswala muhimu yanayo husu kuwatambua wanawake na hakizao.
Hayo yamesemwa na waziri wa ofsi ya rais utumishi CELINA KOMBANI wakati wa hafla ya muendelezo wa sherehe za wanawake ambapo amewawata wanawake kutobweteka na kuhakikisha wanaipigia kura za ndio katiba pendekezwa ili iweze kupitishwa .

Naye waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto SOPHIA SIMBA akizungumza katika hafla hiyo amewataka wanawake kujitokeza katika maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake inayofanyika kitaifa mkoani morogoro ambapo mgeni rasmi atakuwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete.

No comments: