Vifo vingi vya akinamama wajawazito hutokea vijijini kutokana na imani potofu zinazowazuia wanawake kujifungulia hospitali wakiamini watoto wanaozaliwa hospitali hukosa afya hivyo serikali imeombwa kupeleka elimu ya uzazi hasa vijijini ili kuwanusuru wanawake wajawazito na vifo visivyo vya lazima.
Akizungumza na ITV muuguzi mfawidhi katika hospitali ya wilaya ya geita Bi.Anastera Kagya amesema imani potofu zinazotokana na mila zinasababisha kutokea vifo vingi jambo linalokwamisha harakati za kupunguza vifo vinavosababishwa na uzazi.
Awali wakikabidhi zawadi kwa wodi ya wanawake wajawazito ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawakei duniani benki ya CRDB tawi la Geita imekabidhi zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi millioni moja na laki tatu aidha wameziomba taasisi na mashirika mbalimbali kukumbuka kusaidia akinamama wajawazito kutokana na uhitaji wao mkubwa katika kipindi wanachokuwa nacho.
No comments:
Post a Comment