- LEKULE

Breaking

26 Mar 2015



Niaje machalii wangu wa nguvu…inakuwagaje arifu wa kona mbaya kwa fasi ya kitaa hiyo? Kipande hii ni msupa hatare daadeki. Hopu mko biye tangu lasti wiki nilipowasanua dheni nikabonyea kwenye mbishe za kusaka doo. Ama nini? Basi barida! Kaa humu wewe uinjoi udambwidambwi.

Ebana washkaji ishu za politiksi samtaim zinazingua kinoma masela. Si unanyaka kilichohapeni kwa mzazi jembe Zitto? Dah! Yule jombaa ni faita kinoma so huwa sipendagi kichwa kimzingue kabisa kozi kachala ni mzalendo wa ukwehe kabisa! Kama vipi tupa kule ishu fekelo na dosho.

Mazee juzikati si nilitimba kipande hiyo ya Arachuga kwa machalii? Nilitinga kwenye kitu cha msiba wa maza aisee. Soo kama vipi wote tuseme R.I.P kwa mazaa! Ipo dei tutakutana ageini.

Nawu wakati kaka mkubwa nageuza kurejea kwa fasi ya tauni Bongo tambarare pamoko na machungu ya kitu cha msiba ndo listori likahapeni kwenye kitu cha basi mazee.Kama huamini chukua kutoka kwangu. Msela ukikamata ndiga hata siku moko usibane siti ya dirishani kozi lazima atakuja kuchili shori mkareee. Niamini mimi. Hiyo ndo fomula ya masela wa kitaa wewe.

Basi bana, mshkaji kweli akafuzu vigezo na hatimaye shori akaja kukaa siti ya dirishani. Fomula ya kitaa ikawa imefanya kazi.Huku na huku kachaa akaanzisha mastori ya hapa na pale hadi sistaduu mkare akaonekana kama anaelewa somo. Si unajua stori f’lani hivi ameizing.

Wana kitu cha ndinga kikawa kinatambaa hapo rodini dheni mshkaji na shori wakawa wanapokezana tu kitu cha foni wakila mavideo ya gudi miyuziki kwenye haya mafoni ya kuteleza. Chezea kitu cha tachi wewe? Bati usisahau pawa benki kozi hakichelewi kukata chaji aisee.

Ebana drama zilikuwa wakati wa kugonga menyu hapo kwa fasi ya Korogwe. Wakati jamaa anashangaashangaa kwa kuwa hakuwa na mawe ya kumfanyia kufuru mtoto mkare, msela mwingine mwenye kisu si akamchukua shori?

Mazee mtoto alipigwa madikodiko huwezi amini waliporudi kwenye ndinga shori akahamishwa na siti akaenda kuchili na msela baki siti.Aisee msela wa mwanzo alimaindije? Mbaya zaidi yule kachaa aliyechukua mtoto kisu akawa anamfanyia mandingo ya hapa na pale. Mara walaliane mara makisi ya kufa mtu na mavitu mengine ya madizaini hizo.

Duh! Mwanangu akawa amenyang’anywa tonge mdomoni hivihivi kwa kushindwa kuhudumia mzigo. Ndiyo! Ndo kama hivyo unammaindi nini wakati laifu umelikosea mwenyewe mzazi?Nawu deizi tauni unaambiwa kama huna mawe au mabovu ya kutosha basi mashori wote wakare utaishia kuwaita shemeji.

Bati ili kuwa seifu saidi na kuondokana na michongo ya kunyang’anywa mashori kama msela, wewe tafuta mkwanja watakuja wenyewe na taimu hiyo utakuwa unachagua uchukue yupi.

Unanyaka mwana, samtaim msela huwa anajikuta akichukua shori yeyote au hata mbovu kwa kuwa tu hana mauwezo. Sasa chunga situwesheni hiyo isikukute mwana.
Mmenisoma wana? Kama vipi sii yuu neksti wiki! Nduki!

No comments: