Wanananchi wa kijiji cha msisi wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, wameuzuia kwa muda, msafara wa katibu mkuu wa CCM taifa ndugu Abdulrahman Kinana, wakilalamikia vyumba vitatu vya shule iliyoezuliwa paa na upepo tangu mwaka 2011 kutokukarabatiwa, hali iliyo wapelekea wanafunzi wa shule hiyo kusomea chini ya mti na kwenye mahema kwa miaka minne mfululizo.
Wananchi hao wanalalamikia uongozi wa halamshauri ya wilaya ya Bahi na mkoa wa Dodoma kwa kushindwa kukarabati shule hiyo kwa mika minne mfululizo licha ya viongozi wa juu wa mkoa na wilaya na mbunge wao kuwa na taarifa, ambapo wanasema kuwa tangu mwaka 2011, watoto wao wamekuwa wakishindwa kuhudhuria shule vyema na nyakati za mvua na jua kali wanafunzi hupewa likizo ya muda hivyo kuathiri hali ya elimu kwa watoto wao.
Uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, umejukuta na kigugumizi mbele ya umati wa wananchi ulitaka kujua ni lini shule hiyo itakarabatiwa, ambapo katibu mkuu wa CCM taifa ndugu Abdularahman Kinana amewaagiza watendaji kushughulikia tatizo hilo kwani ni la muda mrefu ambapo ameshangazwa na uongozi wa wilaya kukaa kimya kama tatizo hilo hawalioni.
Akiendelea na ziara yake katika mkoa wa Dodoma katibu mkuu huyo wa CCM taifa, alishiriki kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendelo ya wananchi, kushiriki kwenye kilimo, utandazaji wa mabomba ya maji safi, kuhutubia wananchi, ambapo wamewaomba wananchi wa Bahi kutunza Mazingira kwa kuto kata miti ili kuhufadhi mazingira.

No comments:
Post a Comment