Mwenyekiti wa taifa wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema), Mh. Freeman Mbowe amezindua operesheni ya vijana wa chama hicho inayojulikana kama ‘Shahada mkononi delete CCM’ ambayo itasimamiwa na baraza la vijana wa chadema ( Bavicha ), huku akiwataka watanzania kuacha kujengeana chuki za kisiasa na kuwa na upendo kama taifa moja kwani vyama vya siasa ni mambo ya mpito.
Lengo la operesheni hiyo iliyozinduliwa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mahakama ya mwanzo nguzo nane mjini Shinyanga ni kuwahamasisha vijana wenye umri wa kupiga kura kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu, kuwapa fursa wananchi ya kuchagua viongozi bora watakaowaondoa kwenye lindi la umaskini uliokithiri, kuleta haki na usawa kwa watu wote bila ubaguzi pamoja na kujenga jamii iliyo huru kiuchumi kwa kutumia fursa mbalimbali zitokanazo na raslimali za taifa.
Mwenyekiti huyo wa Chadema ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na mbunge wa jimbo la hai mkoani Kilimanjaro, ametumia mkutano huo wa hadhara kuwaasa askari polisi kuacha kutumiwa na chama tawala kuwapiga mabomu na kuwamwagia maji ya kuwasha viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani wakati wanapokuwa katika harakati za kutetea haki za wanyonge, yakiwemo maslahi ya askari polisi kwa madai kuwa serikali ijayo itakuwa ni ya ukawa na wao ndio watakaoendelea kuitumikia.
Uzinduzi wa operesheni hiyo umefanyika sambamba na ugawaji wa baiskeli 17 zilizotolewa na mwenyekiti wa Bavicha taifa Patrobas Katambi kwa uongozi wa kata zote za jimbo la Shinyanga mjini ambazo zitarahisisha zoezi la uhamasishaji wa wananchi kwenda kwenye vituo vya kujiandikisha.

No comments:
Post a Comment