Siku moja baada ya mahakama kuu kutupilia mbali ombi la mbunge wa
Kigoma kaskazini Mh Zitto Kabwe kujadiliwa na vikao vya Chadema kuhusu
hatma ya uanachama wake na kutakiwa kulipagharama za kesi hiyo mbunge
huyo amedai kuzisikia taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na vyombo
vya habari lakini hana taarifa rasmi.
Hayo ndio yalikuwa majibu ya awali ya mbunge huyo wa Kigoma
kaskazini alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya mahakama kutoa uamuzi wake haraka mwanasheria mkuu wa
chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Mh Tundu Lisu akazungumza na
vyombo vya habari kuhusu Chadema kutomtambua Mh Zitto kama mwanachama wa
chama hicho ambapo ili kusikia kauli ya Mh Zitto kuhusu suala hilo ITV
ikafika katika ofisi ndogo za bunge zilizoko jijini Dar es Salaam na
kumshuhudia Mh Zitto akiongoza vikao vya kamati ya kudumu ya bunge ya
hesabu ya mashirika ya uma PAC ambapo baada ya kumalizika kwa kikao
hicho akazungumzia maamuzi hayo ya mahakama na Chadema baada ya kuhojiwa
na waandishi wa habari.
Aidha kutokana na madai hayo Mh Zitto amesema kwa kuwa hana taarifa
rasmi ijumaa ya wiki hii atakwenda jimboni kwake kuzungumza na wananchi
wa jimbo lake kama mbunge na kisha jumanne ya wiki ijayo atahudhuria
vikao vya bunge kama kawaida na kuongeza kuwa tukio hilo linamkomaza
kisiasa na kwamba siasa zake ni zakujadili masuala na si watu kama
walivyo baadhi ya wanasiasa wenzake.
Pia amezungumzia hatma ya mustakabali wake kisiasa na kuelezea
mahusiano yake na chama cha demokrasia namaendeleo Chadema kwa sasa.
No comments:
Post a Comment