Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dk. Wilibrod Silaa amewataka watanzania kubadili fikra zao na kuchagua viongozi wenye fikra sahihi watakaoweza kubadilisha mfumo unaowagandamiza wanyonge na kuwatajirisha wachache ili kubadilisha sura ya Tanzania kwakuwa nchi imebarikiwa na raslimali za aina nyingi lakini haziwanufaishi wananchi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dr. Wilbrod Silaa amewataka watanzania kufungua vichwa vyao kwa wakati huu, taifa linapokabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi, na amesema tatizo halipo katika chama tawala wala serikali iliyoko madarakani, ila tatizo liko kwenye vichwa vya viongozi kushindwa kupanga na kuweka mfumo sahihi wa uongozi, hivyo taifa linahitaji mabadiliko makubwa hali itakayosababisha watanzania kuingia katika hatua nyingine kiuchumi.
Aidha mwenyekiti wa vijana wa Chadema taifa Bw. Patrobas Katambi amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwakuwa kura ndiyo itakayoamua ni jinsi gani ya kutumia raslimali za nchi pale watakapochaguliwa viongozi wenye uchungu na maisha ya watanzania ambao hawafaidiki na kitu chochte mbali na kudanganywa na chumvi, Tsheti, kofia, kanga na vitu vingne ambavyo haviwezi kubadilisha maisha yao.
Awali katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dr. Wilbod Silaa aliwatembelea wahanga walioathirika na mafuriko yaliyosababishwa na mvua ya upepo na mawe katika kijiji cha Mwakata na maguhung’wa na kuwapa pole ambapo alimtaka mkuu wa wilaya ya Kahama Bw Benson Mpesya kuhakikisha kuwa misaada iliyotolewa inagawanywa kwa usawa na haki huku akionyesha masikitiko yake juu ya vitendo vinavyoashiria kuwaongzea maumivu katika mioyo yao wahanga wa tukio hilo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Bw. Benson Mpesya amemueleza katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dr Wilibrod Silaa kuwa watu waliokua wamefunga barabara siku ya tarehe saba asubui kwa lengo la kuishinikiza serikali walikuwa wameletwa kutoka katika vijiji vingine na sio wahanga wa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment