Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia wahamiaji haramu 64 kutoka nchini Ethiopia waliokamatwa katika kijiji cha mkoka wilayani chemba wakiwa safarini kuelekea nchini Malawi ambapo mmoja kati yao amefariki dunia kutokana na njaa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Sacp David Misime akithibitisha kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu amesema waliingia kutokea Tanzania kupitia mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wamepakiwa kwenye gari aina ya Mitsubish fuso lenye namba za usajili T 353 ambalo lilikuwa limebeba magodoro 55 ili kuwaficha wahamiaji hao ambapo gari hilo lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina la Othmani Mteketa liliharibika njiani na ndipo wananchi wakabaini kuwepo kwao na kutoa taarifa polisi.
Aidha kamanda Misime ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa pindi wanapokuwa na mashaka na watu katika maeneo yao ili kuwabaini mapema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Dodoma mjini Betty Mkwasa ametoa wito kwa watu wa mipakani kuwa makini na watu wanaoingia na kutoka nchini kwani haiwezekani watu wakatoka Kilimanjaro hadi Dodoma bila kujulikana.
No comments:
Post a Comment