Wafugaji waomba serikali kugawa maeneo yaliohodhiwa bila kuendelezwa mkoani Morogoro. - LEKULE

Breaking

15 Mar 2015

Wafugaji waomba serikali kugawa maeneo yaliohodhiwa bila kuendelezwa mkoani Morogoro.

Wafugaji mkoani Morogoro wameomba serikali kugawa maeneo ya hifadhi yaliotelekezwa na kuhodhiwa bila kuendelezwa na kuwapa wafugaji ili kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji  inayosabishwa na upungufu wa maeneo ya shughuli za kilimo na ufugaji.

Akizungumza katika mkutano wa chama cha wafugaji na wadau wa mifugo tarafa ya mvuha wilaya ya Morogoro vijijini mkoa Morogoro katibu mkuu wa chama cha wafugaji Tanzania Magembe Makoye amesema kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya mifugo na shughuli za kilimo serikali inatakiwa kuona umuhimu wa kutenge maeneo ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kugawa maeneo ya hifadhi zilizosahaulika yatakayo saidia kupunguza migogoro ya ardhi isiyo ya lazima.

Naye mwenyekiti wa chama hicho George Bajuta amewataka wakulima na wafugaji nchini kuacha mapigano ya mara kwa mara kwani jamii zote zinategemeana na amezitaka jamii za kifugaji kuacha tabia ya kuibiana mifugo kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya wengine na kuhusu utambuzi na tozo kwa mfugaji amesema zoezi hilo haliko lasmi kwani lilianzishwa kwa majalibio katika wilaya tatu ambapo amewataka wafugaji kutojishugulisha na zoezi hilo hadi watakapopata ufafanuzi wake.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa serikali za vijiji na kata akiwemu diwani wa kata ya mvuha Bi,Rehema Hussein akitoa ufafanuzi wa  nani mwenye haki ya kumiliki ardhi kubwa amesema ameshauri chama cha wafugaji kuandaa mpango wa kuelimisha wafugaji wafuge kisasa kwani mifugo inaongezeka kila kukicha lakini ardhi inabaki ileile na hilo litapunguza migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

No comments: