DC MAKONDA AANZA KAZI KWA KISHINDO - LEKULE

Breaking

1 Mar 2015

DC MAKONDA AANZA KAZI KWA KISHINDO




MFUPA uliomshinda Waziri wa zamani wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kuhusu migogoro ya ardhi iliyokithiri katika Manispaa ya Kinondoni Mkuu mpya wa wilaya hiyo Paul Makonda ameahidi kuutafuna.

Makonda ametoa onyo kwa wale wote waliojenga katika maeneo hayo kuanza kuondoka mara moja kabla hawajafikiwa.

"Moto ninaokuja nao katika suala ili hautazimika nitasimamia mimi mwenyewe kwa kushirikiana na polisi ubomoaji wa majengo yote ambayo yamejengwa katika maeneo ya wazi na yale yaliyotengwa kwa ajili ya shule" alisema Makonda.

Makonda alitoa maagizo hayo katika ziara ya siku moja ya kukagua shughuli za maendeleo katika wilaya yake Dar es Salaam jana.

"Mimi simuogopi mtu nasimamia utendaji wangu wa kazi kila mtu anajua msimamo wangu wa kusimamia jambo na katika suala ili hakuna atakaye salimika " alisema Makonda.

Makonda aliagiza migogoro yote ya ardhi ambayo ipo hivi sasa ianze kushughulikiwa na watendaji wanahusika katika manispaa hiyo kuanzia ngazi ya chini na ametenga kila Ijumaa migogoro ambayo inashindikana ipelekwe ofisini kwake ili kuzikutanisha pande zote zinazohusika kwa ajili ya kusuruhisha migogoro hiyo.

Sambamba na agizo hilo Makonga amewataka wote wa manispaa hiyo kusimamia ujenzi wa maabara kikamilifu na kuagiza kuwa Aprili mwaka huu miradi yote iwe imekamilika.

"Hatutasubiri mpaka mwezi wa sita kama alivyo agiza wazirin mkuu kumaliza miradi yote ndani ya kipindi hicho nawaagiza mkamilishe maabara zote ifikapo mwezi wa nne na wale wote watakaoshindwa wajipime utendaji wao" alisema Makonda.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mussa Natty alisema miradi hiyo yote ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari katika wilaya hiyo itagharimu zaidi ya sh. bilioni 2. na kuwa ujenzi wake unasimamiwa na waataalamu waliobobea katika shughuli hiyo.

No comments: