Mechi ya marudiano ya mchujo kuwania Kombe la Klabu Bingwa barani Afrika kati ya El Merrikh ya Sudani na Azam Fc ya Tanzania uliokuwa ukipigwa nchini Sudani umekwisha na matokeo ni kwamba El Merrikh imepata ushindi wa mabao 3-0.
Magoli ya El Merrikh yamepatikana katika dakika za 11, 85 na 90.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam wiki 2 zilizopita Azam ilipata ushindi wa mabao 2-0, kwahiyo El Merrikh imesonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2.
No comments:
Post a Comment