Mkazi mmoja wa Miembe Saba wilayani Kibaha mkoani Pwani
amekamatwa na polisi akituhumiwa kuwabaka watoto wake wawili wadogo kwa
zaidi ya miaka miwili sasa.
Habari zilizolifikia gazeti
hili, zilisema kuwa katika tukio hilo ambalo limethibitishwa na polisi
na watoto wenyewe, baba huyo alianza kuwafanyia binti zake vitendo hivyo
mwaka 2013 kwa siku ambazo mkewe ambaye nimama wa wasichana hao
hakuwapo hadi usiku wa Machi 19, mwaka huu. Kwa sasa tunayahifadhi
majina ya familia hiyo.
Watoto hao mmoja mwenye umri wa
miaka 15 anayesoma darasa la saba na mdogo wake mwenye umri wa miaka 11
aliyeanza kubakwa akiwa darasa la tatu.
Kwa mujibu wa
watoto hao, baba huyo alikuwa anamuita mmoja wa watoto wake chumbani
kwake na kumtaka alale na mdogo wao wa kiume wakati huo akiwa na mwaka
mmoja na binti akipitiwa na usingizi humvua nguo za ndani na kumwingilia
huku akimtaka kukaa kimya na kuvumilia maumivu.
Mke wa
mtuhumiwa huyo, ambaye amekuwa akizimia mara kwa mara kutokana na kulia
baada ya kubaini mchezo huo, alisema aligundua watoto wake wanabakwa
Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa mabinti zake hao kumweleza kuwa baba
yake alikuwa amembaka Machi 19, mwaka huu.
Alisema
kabla ya binti huyo kumweleza hivyo, alimwomba asimpige kwani kuna kitu
anataka amweleze, japo ni kibaya lakini yeye amechoshwa na kimekuwa
kikimuumiza kichwa.
“Alisema kila ninapokwenda katika
biashara zangu, anatamani nisiwe ninawaacha hapo, nikamwahidi sitamfanya
kitu ili mradi aseme ukweli tu,” alisema mama huyo.
Baada
ya kuhakikishiwa kulindwa, ndipo binti huyo aliposimulia jinsi ambavyo
baba yake amekuwa akiwafanyia na kuwatishia wakipiga kelele atawaua.
“Niliposikia
mwili ulisisimka na ghafla binti yangu mwingine naye akatokea akilia na
kuniambia, ‘hata mimi baba ananifanyiaga hivyohivyo kila siku unapokuwa
umepeleka mboga sokoni Kariakoo,” alisema mama huyo.
Mwanamke
huyo ameomba sheria ichukue nafasi yake katika tukio hilo kwa kuwa ni
la kinyama na pia wataalamu wa saikolojia wamsaidie binti yake mdogo wa
darasa la tano kwani yeye ameathirika zaidi.
Daktari aliyewapima watoto hao, ameshauri binti huyo mdogo apate ushauri zaidi ili kurudisha akili yake katika hali ya kawaida.
uu
Simulizi za watoto
Wakizungumza
nyumbani kwao jana watoto hao, walisema baba yao alikuwa akiwatishia
kuwakatakata kwa panga au kuwakaba koo humohumo chumbani endapo
wangethubutu kumweleza mtu yeyote kitendo wanachokifanya.
“Tulikuwa
tumeingia kwetu kulala na wadogo zangu, nikasikia ananiita
nikambembeleze mtoto eti anamsumbua, nilikwenda nikambembeleza akalala,
wakati nashuka kitandani kurudi chumbani kwetu baba akanivuta kwake
akanivua, akasema anachokifanya ni suna kwa hiyo hataki kelele, akisikia
atanikaba nife.”
“Niliumia sana na asubuhi mama
alirudi nikajitahidi kweli asijue na hata shule sikwenda, jioni mama
aliondoka tena baba hakuniita siku hiyo lakini baada ya siku tatu
aliniita tena ikawa vilevile navumilia. Siku zilivyozidi unaweza kukuta
kwa wiki naitwa hata mara nne siku ambazo mama hayupo nyumbani,”
alisema.
Watoto hao walieleza kuwa baadaye baba huyo
alihamia kwa binti mdogo kwa staili ileile na kila mmoja alikuwa akiitwa
kwa zamu na kwa vile kila mmoja alijua ni siri yake na baba. Kutonaka
na woga wa kuuawa, hakuna aliyemweleza mwenzake hadi katikati ya mwaka
jana mmoja wao alipomweleza mwenzake na baadaye kumweleza mama yao.
“Baba
alikuwa anasema atatuua bila hata mtu kujua na tutaozea shambani, hata
nikiwa katika siku zangu baba ananiingilia hivyohivyo, naugua kila mara
UTI, mdogo wangu naye kila mara UTI, tukaamua liwalo na liwe kama kufa
basi ila mama ajue,” alisema mtoto huyo huku akibubujikwa na machozi.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Miembe Saba, Hamis Shomari alisema kabla ya
kupelekwa kituo cha polisi Kongowe Jumamosi iliyopita, watoto hao
waliitwa shuleni hapo na kuhojiwa kila mmoja peke yake na wote walikiri
kuanza kubakwa mwaka 2013 na baba yao na kwamba tabia hiyo iliendelea
hadi Machi 19 usiku alipobakwa binti mdogo kwa mara ya mwisho na Machi
20 walipoamua kumweleza mama yao.
Kamanda wa Polisi
mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema wanamshikilia mtuhumiwa huyo na
kwamba wasichana hao wamefanyiwa vipimo mbalimbali na majibu ya daktari
yamethibitisha kuwa wamebakwa na sehemu zao za siri zimeharibiwa, hivyo
wanaendelea na matibabu.
No comments:
Post a Comment