KOCHA wa ARSENAL , ARSEN WENGER amelalamikia safu ya ulinzi ya timu yake kwamba haikuwa makini kuwazuia wachezaji wa MONACO katika mchezo ambao ARSENAL kwa mara nyingine tena ilishindwa kutamba katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barai ulaya kufuatia kufungwa bao 3-1 dhidi ya MONACO kwenye uwanja wa EMIRATES.
The GUNNERS wameingia katika mchezo huo wakiwa wanapewa kipaumbele cha kuibuka na ushindi lakini walianza kujikuta wakiwa nyuma kwenye dakika ya 38 pale GEOFREY KONDOBIA alipoanza kuandika bao la kwanza.
Wenyeji wa uwanja wa EMIRATES ARSENAL walipata nafasi kadhaa za kufunga kupitia kwa OLIVIER GIIROUD lakini walishindwa kuzitumia vyema.
MONACO kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa TOTTENHAM HOTSPURS DIMITAR BERBATOV waliongeza bao la pili kwenye dakika ya 53 kabla ya ALEX OXLADE CHAMBERLAIN aliyeingia kipindi cha pili kuipatia timu yake ya ARSENAL bao la kwanza kwenye dakika ya 90.
Zikiwa zimesalia sekunde mpira kumalizika FERREIRA CARASO wa MONACO aliongeza bao la tatu na kuifanya ARSENAL kuwa na mlima wa kupanda katika mchezo wa duru la pili mjini MONACO kama itataka kufuzu hatua ya robo fainali.

No comments:
Post a Comment