Mbwa mmoja wa Polisi huko New Jersey Marekani wenye umri wa miaka nane aliyefanya kazi kwa miaka minne amelazimika kustaafu kutokana na afya yake kuwa mbaya.
Mbwa huyo wa Polisi ambaye anaitwa Judge amepewa heshima na kuagwa kishujaa, kaandaliwa na gwaride pamoja na kupigiwa saluti na Polisi tukio ambalo lilishuhudiwa pia watu wa haki za wanyama.
Judge alikuwa anastaafu kama mbwa
wa Polisi kwenye kituo kimoja West Deptford, New Jersey ambapo alitakiwa
kustaafu tangu mwaka 2013, kutokana na maradhi ya meno na pia afya yake
kuwa sio nzuri.
Watu wa haki za wanyama walishauri mbwa huyo ‘astaafishwe’ na pia apelekwe kupatiwa matibabu katika Hospitali ya wanyama ya Swedesboro.
Huu ni msafara wa gari zilizombeba mbwa huyo
Tukio hilo sio geni sana kwa wenzetu, kuliwahi kuwa na story ya ishu ya mbwa mmoja wa Polisi ambaye alizikwa kwa heshima kama ambavyo huwa mazishi ya askari yanafanyika.
Shughuli za mazishi ya mbwa.
No comments:
Post a Comment