Mkoa wa Njombe umeelezwa kwamba ni miongoni mwa mikoa itakayoliwezesha taifa la tanzania kukua zaidi kiuchumi na kuwa na uchumi wa kati ama mkubwa endapo itatumia ipasavyo rasilimali zake mbalimbali zilizopo ikiwemo makaa ya mawe na chuma yaliyopo liganga katika wilaya yaludewa.
Akizungumza katika kikao cha kamati cha ushauri (RCC) cha mkoa wa njombe,mkuu wa mkoa huo Dkt. Rehema Nchimbi amesema kuna uwezekano mkubwa wa taifa la Tanzania kukua zaidi kiuchumi na kuwa na uchumi wa kati ama mkubwa akilinganisha na mataifa makubwa ikiwemo china endapo litaamua kutumia vyema rasilimali za mkoa wa njombe ikiwemo makaa ya mawe na chuma.
Mkoa wa njombe unaotimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake na kuzinduliwa na rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania, mh. Dkt. Jakaya Kikwete octoba 18 mwaka 2013, ni miongoni mwa mikoa inayotarajiwa kukua zaidi kiuchumi lakini tatizo kubwa ni kuwepo kwa bajeti zisizotekelezeka.
Deo Haule Filikunjombe ni mbunge wa jimbo la Ludewa, anasema pamoja na mkoa wa njombe kujaaliwa kuwa na wabunge wengi mawaziri lakini anasikitishwa na kukwama kwa mipango mingi ya kuendeleza mkoa huo jambo ambalo anasema linatokana na wengi wao kuwa walalamikaji zaidi badala ya utendaji.
Aidha, Filikunjombe ametumia kikao hicho cha RCC njombe, kukemea vikali vitendo vya kikatili dhidi ya watoto na watu wenye ulemavu wa ngozi huku akimuomba mkuu wa mkoa wa njombe kuandika waraka sehemu zote za mashule, makanisa na misikiti kueleza ubaya wa vitendo hivyo.

No comments:
Post a Comment