Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi (TAS) mkoa wa Ruvuma, kinatarajia kufanya maandamano ya amani machi 2 mwaka huu kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuishinikiza serikali kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na kubainika na tuhuma za kuhusika na mauaji ya albino kwa madai kwamba baadhi yao wamekamatwa lakini mwenendo wa kesi zao bado haueleweki.
Akizungumza na ITV katibu mtendaji wa chama cha walemavu wa ngozi mkoa wa Ruvuma, Amini Mkapunda, pamoja na kulaani matukio kadhaa ya kikatili ikiwemo mauaji ya watu wenye Albinism kwa vigezo vya kutafuta utajiri ama nafasi mbalimbali za kisiasa kwa imani za kishirikina, amesema ifike wakati serikali ichukue hatua kali kwa wahusika kuliko hali ilivyo sasa.
Mauaji ya Albino na wazee hapa nchini yote yamekuwa yakihusishwa na imani za kishirikina, jambo ambalo afisa mtendaji mkuu wa shirika la kuhudumia wazee Tanzania (PADI) Iskaka Msigwa pamoja na mwenyekiri wa shirika la ROA, Mathew Ngalimanayo wanasema hii yote inatokana na jamii kukosa hofu ya mungu na wakati mwingine yanahusisha familia husika.
Pamoja na kutokuwepo kwa matukio ya mauaji ya Albino kwa mkoa wa Ruvuma lakini jeshi la polisi mkoani hapa linalaani vitendo hivyo na kwamba halitasita kuwachukulia hatua kali wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

No comments:
Post a Comment