Wakereketwa wa haki za binadamu
nchini Uganda wanawashutumu polisi wa nchi hiyo, kwa kuwanyanyasa na
kuwapiga wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Kundi hilo
liitwalo Chapter Four Uganda, linasema limeorodhesha visa kadhaa ambavyo
polisi wanawalazimisha wanaume kuvua nguo zao na kubaki uchi, ili
kuonyesha sehemu zao nyeti kubaini iwapo wanahusika katika matendo hayo
ya ngono ya jinsia moja.Waziri wa msawala ya ndani nchini Uganda Jenerali Aronda Nyakairima, ameiambia BBC kuwa madai hayo si ya kweli, lakini akasema kuwa afisi yake itayachunguza.
Mapenzi ya jinsia moja ni marufuku nchini Uganda, lakini serikali ina mpango wa kuanzisha sheria kali zaidi.
No comments:
Post a Comment