Fidia ya Maumau yafarakanisha Ndoa Kenya - LEKULE

Breaking

27 Feb 2015

Fidia ya Maumau yafarakanisha Ndoa Kenya

Thedrinah Wanjiru na Lawrence Kairianja ni miongoni mwa Wapenzi walioapa kuishi pamoja mpaka kifo kitakapowatenganisha.

Lakini Bibi Wanjiru mwenye umri wa miaka 80 kutoka Nyeri, aliamua kutengua kiapo hicho kwa kuachana na mumewe mwenye umri wa miaka 82 baada ya kulipwa pesa ya fidia akiwa mmoja kati ya Wakenya walioathirika na vita vya Mau mau.

Wanjiru alimfukuza nyumbani mumewe baada ya kupokea kiasi cha shilingi 400,000 za Kenya.

Wapenzi hao wamedumu kwenye ndoa kwa miaka 63.

Hata hivyo, Wazee waliingilia kati mzozo huo na kumlazimisha Bibi Wanjiru kukabidhi baadhi ya nyaraka za mumewe.

Tangu alipopata pesa hizo Bibi huyo alibadili mtondo wa maisha yake yaliyopambwa na fedha na dhahabu.

Bernard Mwangi, mmoja kati ya Watoto wao alisema kuwa ndugu zake pia na mama yake wamekuwa wakitumia hela jijini Nairobi na Miji mingine, wakimuacha yeye na Baba yake Mzee nyumbani bila chakula
Enzi za ujana wao Bibi Thedrinah na Lawrence 

Mateso

''tangu walipopata pesa, Mama yangu na Kaka zangu wamekuwa wakitutesa, natamani wangeniacha mimi na kumpa Baba yangu pesa'' alieleza Mwangi.

Baadhi ya Watoto wa Kairianja waliungana na Mamam na kumtimua Baba yao, ambaye sasa anaishi Nyumba ya jirani yao.

Alipotafutwa kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo Wanjiru alisema anampenda mumewe na angependwa kuwa naye tena.

''ni kweli tulipokea kiasi hicho cha pesa, tumekuwa tukitumia pamoja na mume wangu, nina muhitaji tena ingawa amekuwa akinitendea isivyo pia alipokuwa akifanya kazi Nairobi.Aliniacha nyumbani peke yangu bila Chakula kwa ajili ya Watoto na sasa anadai anaonewa?'' aliuliza Bibi Wanjiru.

Baadhi ya Wanafamilia wamekataa kuingilia kati mzozo huo na kuwaunganisha wapenzi hao wakidai kuwa kitando alichokifanya Wanjiru ni laana.

Kaka wa Kairianja, Daniel Wanjohi amesema hawatamruhusu Wanjiru kurudiana na mumewe hata kama akirudi kuomba radhi, na kuongeza kuwa Dhamira ya Watoto walioungana na Mama yao itawarudisha kwa Baba yao.

No comments: