Baada ya kushinda mechi 10 mfululizo katika siku za hivi karibuni – FC Barcelona wakiwa na kikosi chao kilichosheheni mastaa leo kilipambana na Malaga katika mfululizo wa mechi za ligi kuu ya Hispania.
Mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Camp Nou – tumeshuhudia Barca wakipunguzwa kasi kwa kushindwa kupata ushindi ambao ungewapeleka kwenye usukani mwa ligi hiyo.
Malaga leo hii wamefanikiwa kuinyoosha FC Barcelona kwa kipigo cha 1-0.
Goli la mapema kabisa katika kipindi cha kwanza lilofungwa na Juanmi lilitosha kuipa ushindi muhimu Malaga dhidi ya kikosi cha Luis Enrique.
Lionel Messi ambaye amefunga magoli 12 katika mechi 8 zilizopita leo alikosa kabisa cheche za kuipita ngome ya Malaga.
Kwa matokeo hayo Barcelona wamebaki nafasi ya pili kwenye ligi wakiwa na pointi moja nyuma ya vinara Madrid ambao wanacheza kesho dhidi ya Elche.
No comments:
Post a Comment