Jeshi la Nigeria linasema kuwa
limeukomboa mji wa Baga, kaskazini mashariki mwa nchi ambako mamia ya
watu waliuliwa na kundi la Boko Haram mwezi uliopita.
Jeshi lilisema kumetokea mapambano makali na wapiganaji hao Waislamu na hasara ilikuwa kubwa.Shirika la kutetea haki za kibinaadamu, Amnesty International, lilisema kuwa watu kama 2,000 waliuwawa Boko Haram ilipoiteka Baga - shambulio lao kubwa kabisa.
Serikali ya Nigeria ilisema watu 150 walikufa katika mji huo.
Baga iko kando ya Ziwa Chad kwenye jimbo la Borno - Boko Haram waliposhambulia maelfu ya watu walivuka ziwa kutafuta hifadhi nchini Chad.
No comments:
Post a Comment