KESI YA CHID BENZ YAAHIRISHWA HADI APRILI 26 - LEKULE

Breaking

23 Feb 2015

KESI YA CHID BENZ YAAHIRISHWA HADI APRILI 26


Kesi inayomkabili mwanamuziki Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ akidaiwa kukutwa na madawa za kulevya leo imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam hadi Aprili Aprili 26 mwaka huu.

Kesi hiyo imeahirishwa baada ya polisi kutowasilisha jalada katika mahakama ambapo wakili wa serikali, Diana Luhongo, alisema jalada la  maelezo ya awali la mshtakiwa halijawasilishwa mahakamani.

Mwanamuziki huyo ansdaiwa kukamatwa mwaka jana uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya wakati akijitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.

No comments: