Hakimu Ngomero aliongeza kwa kusema kuwa, kutokana na kitendo cha kinyama alichokifanya Shija cha kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 5, mahakama hiyo imelazimika kumhukumu kifungo cha maisha jela. Awali Mwendesha Mashitaka wa Serikali wilayani Nzega Melito Ukongoji aliiambia mahakama hiyo kuwa, mnamo Mei 19, 2014 katika Kijiji cha Kidete wilayani Nzega saa 8 mchana, Shija alifumaniwa chini ya mti wa mwembe akiwa anambaka mtoto huyo. Aidha Melito aliongeza kuwa kutokana na kitendo alichokifanya mtuhumiwa kilimsababishia mtoto huyo maumivu makali katika mwili wake pamoja na kutoka damu nyingi. Mwendesha Mashitaka huyo, aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo kutokana na kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa cha kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 5. Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, mahakama hiyo ilitoa nafasi ya utetezi kwa mtuhumiwa ambapo aliiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu kutokana na kuwa mwathirika wa virusi vya Ukimwi. - LEKULE

Breaking

23 Feb 2015

Hakimu Ngomero aliongeza kwa kusema kuwa, kutokana na kitendo cha kinyama alichokifanya Shija cha kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 5, mahakama hiyo imelazimika kumhukumu kifungo cha maisha jela. Awali Mwendesha Mashitaka wa Serikali wilayani Nzega Melito Ukongoji aliiambia mahakama hiyo kuwa, mnamo Mei 19, 2014 katika Kijiji cha Kidete wilayani Nzega saa 8 mchana, Shija alifumaniwa chini ya mti wa mwembe akiwa anambaka mtoto huyo. Aidha Melito aliongeza kuwa kutokana na kitendo alichokifanya mtuhumiwa kilimsababishia mtoto huyo maumivu makali katika mwili wake pamoja na kutoka damu nyingi. Mwendesha Mashitaka huyo, aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo kutokana na kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa cha kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 5. Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, mahakama hiyo ilitoa nafasi ya utetezi kwa mtuhumiwa ambapo aliiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu kutokana na kuwa mwathirika wa virusi vya Ukimwi.


WAZIRI wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dk John Pombe Magufuli amelaani vikali tukio la kikatili la kutekwa na kuuawa kwa mtoto Yohana Bahati pamoja na kujeruhiwa vibaya kwa mama mzazi wa marehemu na watu wasiofahamika.
 
Akizungumza kwa masikitiko makubwa jijini Dar es Salaam, Dk Magufuli amewataka Watanzania kuishi kwa amani na upendo na kuacha dhana ya kutajirika kutokana na viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
 
“Tukio hili ni la kinyama na halikubaliki popote duniani, watu wanatakiwa waelewe kuwa mtu huwezi kutajirika kutokana na viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi kama alivyofanyiwa mtoto Bahati,” alisema Waziri Magufuli.
 
Katika hatua nyingine, Waziri Magufuli ametoa msaada wake wa awali kiasi cha Sh milioni moja kwa ajili ya kumsaidia Ester Jonas mama mzazi wa mtoto huyo aliyeuawa na watu hao wasiofahamika.
 
“Nimeona nitoe msaada wangu wa awali kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kumsaidia mama huyu aliyejeruhiwa vibaya kwa ajili ya mahitaji yake mbalimbali na hapo baadaye nitakapopata nafasi nitakwenda nyumbani kwake kutoa pole zaidi,” alisema Waziri Magufuli.

No comments: