HALIMASHAURI ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga imewaonya walimu wa shule za msingi wanaopuuza agizo la serikali la kuzuia kuwarudisha nyumbani wanafuzi ambao wazazi wao wanashindwa kuwalipia michango mbalimbali ambayo imezuiwa na serikali
Kauli hiyo imetolewa na afisa elimu wa shule za msingi katika halmashauri ya mji wa Kahama Bw. Aruko Lukolela baada ya kuwepo malalamiko ya wazazi katika shule za msingi za Nyasubi na Mbulu ambako imedaiwa baadhi ya wanafunzi kurudishwa nyumbani kwa kukosa fedha hizo.
Amesema hakuna utaratibu wa kiserikali wa kumrudisha mwanafunzi nyumbani kwa kukosa michango kwa kuwa serikali ilikwisha futa michango yote kwenye shule za msingi na elimu hiyo hutolewa bure nchini.
Amewataka walimu wanaowachangisha wanafunzi kuacha mara moja na atakaebainika kuendelea kuwachangisha wazazi atachukuliwa hatua za kisheria , wakiwemo wanaodai fedha wakati wa kuwaandikisha watoto darasa la kwanza au awali kwa kuwa wanatakiwa kuandikishwa bure.
Awali mmoja wa wadau wa elimu wilayani Kahama Bw. Joseph Chimakaguli amesema walimu hao wamekuwa wakifanya biashara ya Fulana (T-Shirts) ambazo madukani huuzwa shilingi elfu moja na mia tano lakini wao wamekuwa wakiwauzia wazazi kwa shilingi elfu saba kwa fulana hali ambayo amedai inastahili kuachwa kwa walezi na wazazi wenyewe kununua madukani.
No comments:
Post a Comment