Huku kukiwa na tabia kuwa baadhi ya wanawake
wanapokuwa wajawazito wanakuwa na tabia za kusumbua na kubagua baadhi ya
vitu, msanii wa filamu za Kibongo Aunty Ezekiel ‘Mama Kijacho’, amesema
kwa upande wake yuko vile vile na wala hajabadilika.
Akiongea na mpekuzi, Aunty alisema kuwa haoni kama amebadilika
kitabia au kuwa msumbufu bali anajiona yupo kawaida ingawa mara nyingine
anakuwa anachoka sana
“Mimba wala haijanibadili maisha kwa maana sipo kama wanawake wengine wanavyokuwa wasumbufu, naamini kuwa nitaendelea kuwa hivi hadi mwisho nitakapojifungua,” alisema Aunty.
No comments:
Post a Comment