Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha
nchini Msumbiji zimesababisha maafa makubwa ambapo watu kadhaa
wamefariki na wengine kupoteza makazi yao.
Serikali ya Msumbiji
imetoa tahadhari ya hali ya juu kwenye eneo la kaskazini na katikati mwa
nchi hiyo kufuatia mafuriko yaliyotokana na mvua hizo.Hadi sasa watoto 18 hawajuliani walipo na kuna taarifa watu kadhaa wamesombwa na maji yaliyokuwa yakitiririka katika mto mmoja.
Mawasiliano ya barabara inayounganisha eneo la kati na kaskazini mwa nchi hiyo yameharibika.
No comments:
Post a Comment