Mistari mirefu imeshuhudiwa katika vituo vya kuuza magazeti nchini Ufaransa huku mamia ya watu wakitaka kujipatia nakala jipya la gazeti la Charlie Hebdo.
Nakala milioni 5 zimechapishwa , wiki moja baada ya vijana wawili wa kiisilamu kuwaua watu 12 katika ofisi za jarida hilo pamoja na watu wnegine watano katika mashambulizi tofauti mjini Paris.
Jarida hilo limechapisha kibonzo kinachomuonyesha Mtume Muhammad akilia huku akishikilia bango linalosema ''mimi ni Charlie''.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al-Qaeda nchini Yemen, limedai kuhusika na mashambulizi yaliyofanyika dhidi ya jarida hilo.
Katika video ya dakika 12 iliyowekwa kwenye akaunti rasmi ya twitter ya wanamgambo hao wa AQAP, kiongozi wa kundi hilo anasema walipanga nani alengwe na hata kufadhili operation yote katika offisi za Charlie Hebdo.
Anasema aliyeamuru hilo kutekelezwa ni Ayman al-Zawahiri,mtu aliyemrithi marehemu Osama bin Laden aliekuwa kiongozi mkuu wa Al Qaeda .
Uhusiano kati ya kaka wawili waliofanya mashambulio hayo na AQAP ulikua tayari umebainika.
Hata hivyo ukanda huo wa video ni thibitisho kamili kwamba AQAP - ambayo Marekani wamekuwa wakiwataja kama kundi kali zaidi miongoni mwa makundi kadhaa ya wanamgambo wa kiislamu, linaweza kushambulia kwa namna ambayo wengine huenda wasiweze, licha ya kuwa halijajulikana sana kama lile kundi la Islamic state.
La kutiwa wasiwasi zaidi ni kuwa katika picha ya kanda hii ya video kiongozi huyo wa AQAP anaonekana akisimama kando ya bendera ya IS.
No comments:
Post a Comment