Kijana huyo alipigia polisi simu na kuwaambia kwamba angependa waende nyumbani kwake huku wakiandamana na wataalamu wa uchunguzi wa mauaji kwani alikuwa amemuua rafiki yake. .
Kijana huyo kwa jina Lewis Daynes mwenye umri wa miaka 19 , ametajwa na polisi kuwa kijana hatari, mhalifu ambaye anawahadaa wenzake na kisha kuwadhuru.
Inaarifiwa ilikuwa mara ya kwanza kwa wawili hawa kukutana uso kwa uso kwani suiku zote mawasiliano yao yalikuwa kupitia internet.
Daynes, alifungwa jela maisha baada ya kiupatikana na hatia ya kumuua Breck Bednar mwaja jana.
Daynes kutoka Grays, Essex, alimwalika Bednar nyumbani kwake baada ya kujuana tu kupitia internet akiwambia alitaka sana kumuona. Bedner alipowasili nyumbani kwa Daynes, Daynes alimfunga mikono yake na kisha kumuua.
Taarifa hii ya kijana huyo kuwapigia polisi simu na kuwaarifu kuhusu mauaji aliyoyafanya, imeibuka hii leo siku moja baada ya hukumu kutolewa dhidi yake.
'ninahitaji polisi kuja nyumbani kwangu,'' alisema kijana huyo na alipoulizwa ikiwa alikuwa anakiri kufanya mauaji akaseme, '' Ndio , ninakiri. ''
Baadaye aliwapa polisi taarifa zake, jina lake na alikoishi na kisha kuwashukuru. Alidai kwamba alimuua rafiki yake Breck baada ya kumtisha kwa kisu.
''Sikumbuki kilichotokea lakini nilimchinja, '' aliwaambia polisi.
Baadaye polisi walifika nyumbani kwake na kumpata Daynes akiwa mtulivu huku mwili wa rafiki yake ukiwa sakafuni.
Daynes, ametajwa kama kijana ambaye hakueleweka kitabia ila alipenda sana kutumia muda wake kwenye kompiuta. Wazazi wake waliachana hali iliyosababisha maafisa wanaoshughulika maslahi ya watoto kumpeleka kwa familia ambayo sio yake ili aweze kutuzwa.
Alikatakata nguo alizokuwa amezivaa akijaribu kuharibu komputa aliyokuwa anaitumia ili kufuta ushahidi wa mazungumzo waliyokuwa nayo na rafiki yake kabla ya kumuua.
Kabla ya kuwapigia polisi simu, alimtumia mtu mmoja picha ya mwili wa Bednar ushahidi wake kwamba amemuua. Hata hivyo polisi wangali wanachungaza kumtambua mtu huyo.
Mamake kijana aliyeuawa amesema anatuami kuwa kisa cha mwanake kitakuwa funzo kwa vijana wanaojihusisha na michezo ya kwenye internet.
No comments:
Post a Comment