Mahakama moja ya Misri imelipiga marufuku tawi la kundi la Palestina Hamas nchini humo na kuliorodhesha kama kundi la kigaidi.
Kundi la Hamas ndilo linaloongoza mashambulizi katika eneo la Gaza na maafisa wa Misri wanadai kwamba silaha hutolewa katika eneo hilo na kusafrishwa hadi eneo la Sinai ambapo Misri inakabiliana na wapiganaji.
Marufuku hiyo inajiri siku kadhaa baada ya wapiganaji hao wa kiislamu kuanzisha mashambulizi ya maafisa wa polisi na wanajeshi katika mkono huo wa bahari na kuwaua takriban watu 30.
Hamas imepinga marufuku hiyo ya mahakama ikiitaja kuwa ya kisiasa
No comments:
Post a Comment