Umoja wa Afrika umetishia pande mbili zinazopigana Sudan Kusini kwamba zitawekewa vikwazo.
Baraza la Amani na Usalama la AU limesema vikwazo vitawekwa kwa pande zote ambazo zinachafua makubaliano ya amani.
Piya liliomba serikali na wapiganaji kueleza mapendekezo yao kuhusu serikali ya mpito kabla ya mkutano wa viongozi wa AU kumalizika mjini Addis Ababa.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na jumuia ya Afrika Mashariki, IGAD, piya zimetishia kuwa zitaweka vikwazo.
Mapigano yalianza mwaka 2013 baina ya wanajeshi wa Rais Salva Kiir na wale watiifu kwa makamo wake wa rais wa zamani, Riek Machar.
Mapigano yameendelea ingawa makubaliano kadha ya amani yametiwa saini
No comments:
Post a Comment